Home Habari za michezo ‘MAVITUZI’ YA OUATTARA YAMTIA WAZIMU ZORAN…AFUNGUKA NAMNA ATAKAVYOMTUMIA KIMKAKATI KUMALIZA ‘KAZI CHAFU’…

‘MAVITUZI’ YA OUATTARA YAMTIA WAZIMU ZORAN…AFUNGUKA NAMNA ATAKAVYOMTUMIA KIMKAKATI KUMALIZA ‘KAZI CHAFU’…


Beki mpya wa kati Simba, Mohamed Ouattara juzi alicheza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Al Akhdood na Simba kushinda mabao 6-0 na kumpasua kichwa kocha Zoran Maki ambaye amepata akili mpya ya namna ya kumtumia kwa pamoja na ukuta ule wa Henock Inonga na Joash Onyango.

Ouattara aliingia kipindi cha pili alitumika nafasi mbili akianza kama beki wa kati akicheza na Joash Onyango kisha kumaliza mchezo eneo la kiungo mkabaji na kote alifanya vizuri.

Kocha Mkuu wa Simba, Zoran Maki alisema ushindi huo ni kitu kikubwa, lakini kuona wachezaji wake wameimarika maeneo gani na wapi kwenye upungufu anakotakiwa kufanyia kazi.

Alisema ushindi unaleta hali ya kujiamini kwa wachezaji na vichwani mwao kuamini kila mechi kuwa wanastahili kushinda.

Alisema bado timu haijafikia kiwango anachotaka, lakini wachezaji wameanza kuzoeana, kuelewa mazoezi anayowapa na baada ya kumaliza maandalizi hayo atakuwa na kikosi imara.

“Kuhusu Ouattara uwepo wa mchezaji wa daraja lake ndani ya kikosi chetu ni faida kubwa kwani ana uwezo mzuri wa kucheza beki wa kati na kutimiza majukumu ya kiulinzi,” alisema Zoran.

“Faida nyingine ya Ouattara ni kucheza kiungo mkabaji. Ana uwezo mkubwa na hilo kila mmoja atakuja kuliona kwenye michezo ya mashindano ila kuhusu kucheza kikosi cha kwanza hilo sio rahisi kwani Onyango na Henock Inonga nao wapo kwenye ubora.

“Ushindani kati yao watatu Ouattara, Inonga na Onyango wawili watakaokuwa bora zaidi katika maandalizi ya mchezo husika watapata nafasi.”

SOMA NA HII  MZEE WA JAMBIA AIKATAA YANGA KIMATAIFA....''WAKIFUZU ROBO FAINAL ITAKUWA BAHATI KWAO''...