Home Uncategorized BONDIA ALIYEIABISHISHA TANZANIA KUCHUKULIWA HATUA – MWAKYEMBE

BONDIA ALIYEIABISHISHA TANZANIA KUCHUKULIWA HATUA – MWAKYEMBE


Watanzania wanajadili ni kipi cha kufanya juu ya mmoja wa wachezaji ndondi wake mashuhuri baada ya kukatiza mpambano nchini Australia katika raundi ya pili bila kukuonyesha juhudi zozote.

Ilikuwa ni raundiya tatu kuwahi kuchezwa na Selemani Bangaiza katika ndondi za uzani wa super flyweight nje ya Tanzania na aliwekwa baadae kama mchezaji ambaye angekaba nafasi hiyo kukabiliana na Andrew Moloney ambaye hajawahi kupigwa.

Mazungumzo juu ya mwanamasumbwi huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 20-yanafanyika baada ya Waziri wa michezo wa Tanzania Harrison Mwakyembe kutitaka shirikisho la mchezo wa ndondi nchini humo kumuadhibu mwanamasumbwi Selemani Bangaiza kwa kukatiza mapigano katika raundi ya pili, ameieleza BBC mkuu wa shirikisho hilo.

Waziri anadhani Bangaiza angeruhusiwa kupigana tena baada ya kutazama video ya mpambano ambayo ilizagaa kwenye mitandao ya habari ya kijamii.

Katika video hiyo, Bangaiza anaonekana akishika mikono yake na kutoa ulimi kuonyesha ishara kuwa hakutaka kundelea na mpambano:

Joe Anea, rais wa tume ya mchezo wa ndondi (TPBRC), ameiambia BBC kuwa waziri wa michezo alitaka Bangaiza aadhibiwe kwasababu hakuwa na sababu nzuri ya kukatiza mchezo.

TPBRC inajadili ikiwa Bangaiza ataadhibiwa au la.

Bwana Mwakyembeamemshutumu bondia huyo kwa kutojitahidi kwa kutosha na kutoiwakilisha Tanzania vema.

“Mambo kama haya yanaifanya nchi yetu kuonekana kuwa nyuma kimichezo ,” Alinukuliwa waziri akisema katika gazeti hilo.

“Bondia huyo anapaswa kuondolewa ili iwe funzo kwa wengine.”

Bondia wa uzani wa super flyweight alimpiga Selemani Bangaiza, na kumlazimisha kuondoka ulingoni katika raundi ya Jumamosi jioni katika uwanja wa klabu ya Ragbi wa Seagulls Rugby katika eneo la Tweed Heads, New South Wales, Australia.

Moloney alizipiga ndondi hizo baada ya kupata ushindi kwa nokauti kunako raundi ya 8 dhidi ya Miguel Gonzalez mwezi Machi nchini Chile.

Ushindi wake unamfanya kuwa bondia ambaye hajawahi kushindwa.

Bangaiza aliingia ulingoni akiwa mwenye kujawa na tabasamu, lakini matokeo hayakuwa mazuri baada ya kipenga cha kuanza mchezo kupigwa mchezo wake ulikuwa ni wa pili tu nje ya Tanzania, ambapo safari yake ya kwanza ya ndondi nje ya nchi ilimpeleka Afrika kusini.

SOMA NA HII  YANGA YATUMA UJUMBE MZITO KWA SIMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here