Home Uncategorized GLOBAL FC YATUMA SALAMU E MEDIA

GLOBAL FC YATUMA SALAMU E MEDIA


 KUELEKEA kwenye mechi ya kirafiki kati ya wababe wa mji Global FC dhidi ya E Media, Kocha Mkuu wa kikosi cha Global FC, Philip Nkini amesema kuwa wamejipanga kuwafunga E Media pamoja na wachezaji wao.

Leo Oktoba 23, Global FC wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya E Media kwenye Uwanja wa Tanganyika Packers wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 4-1 kwenye mchezo uliopita wa kirafiki na Azam Media.

Nkini ameieleza Spoti Xtra kuwa wamejiandaa vema katika kukifunga kikosi cha E Media na kuweza kurudisha heshima kwa timu inayotumia wachezaji halali wa Kampuni ya Global.

“Ninafahamu kuwa wachezaji wengi wa E Media wanatoka nje na kufanya kikosi chao kionekane bora kuliko timu nyingine zote. Sisi tunawachezaji wa hapa hapa ndani, hawatutishi.

“Kwenye mchezo wetu uliopita changamoto kubwa ilikuwa ni kipa. Kipa wetu alikuwa safarini kwenye majukumu ila sasa amerejea rasmi. Hivyo, kwenye mechi ya kesho, kikosi cha Global kitalindwa na kipa mwenye ubora wa kimataifa,” alisema Nkini.

SOMA NA HII  VIDEO: MEDDIE KAGERE AKIJIFUA SEBULENI