Home Uncategorized HAKIKA MAJOGOO WAMEAMUA, JURGEN KLOPP KUSHUSHA MASHINE NYINGINE KALI LIVERPOOL

HAKIKA MAJOGOO WAMEAMUA, JURGEN KLOPP KUSHUSHA MASHINE NYINGINE KALI LIVERPOOL


Kocha wa liver, Jurgen Klopp amechimba mkwara kuwa timu yake itashusha mastaa wengine wa hatari ili kuimarisha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao. Liverpool katika siku za karibuni imekuwa miongoni mwa timu zinazomwaga fedha nyingi katika usajili.

Klopp alisema kuwa timu hiyo baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya inataka kujiimarisha zaidi. Kocha huyo amesema ni lazima klabu hiyo isajili mastaa zaidi ili iweze kufanya vizuri msimu ujao itakapotetea taji lao la Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia kupigania ubingwa wa Ligi Kuu England.

“Liverpool tunataka mafanikio zaidi kwa hiyo tupo tayari kutumia pesa zaidi ili kutimiza ndoto zetu,” alisema Klopp, ambaye ana kibarua cha kuongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa England iliyoutwaa mara ya mwisho msimu wa 1989/90.

Liverpool ina beki ghali zaidi duniani, ambaye ni Virgil van Dijk, ambaye ilimnunua kwa kitita cha pauni milioni 75 (Sh. bilioni 218) na kipa ghali wa pili duniani, Alisson, ambaye walimsajili kwa pauni milioni 66 (Sh. bilioni 192).

SOMA NA HII  KOBE BYRANT AZIKWA KWA SIRI