Home Burudani HILI JIPYA LA Infinix SIO LA KUPUUZA…SAFARI HII NI MWENDO WA KUISHI...

HILI JIPYA LA Infinix SIO LA KUPUUZA…SAFARI HII NI MWENDO WA KUISHI KISTAA ZAIDI KAMA ZUCHU NA MEENA ALLY…

 


Je unafahamu kuwa Infinix NOTE 12 au HOT 12 1 tu inaweza kukupa Smart TV, Laptop(Computa), King’amuzi cha DSTV na zawadi nyingine nyingi. 

Hii ni kwa wajanja wote wenye kuishi kiVIP, Kampuni ya simu Infinix imezindua rasmi promosheni kubwa ya Mwaka ambayo imekuwa ikifanyika kila Mwaka mara moja yenye kufahamika kama “KALIKULIKO2022”. 

Promosheni ya Infinix Kalikuliko itadumu kwa kipindi cha Mwezi mmoja imeanza Tarehe 6 ya Mwezi huu na hitimisho ni Tarehe 6 ya Mwezi wa 9.

Kwa mujibu wa Meneja Mauzo Jackline Steven alidai kuwa, “katika kipindi hiki chote cha Mwezi mmoja wateja wote wa simu za Infinix hawataondoka dukani mikoni mitupi ni nunua tukuzawadie papo hapo na tukuingize katika droo kubwa ya kila Wiki ujishindie TV, Laptop, King’amuzi cha DSTV na zawadi nyengine nyingi ikiwamo punguzo la bei utakalohitaji wewe mteja wetu”,


Aliongeza, “simu ambazo zitakuwa katika promosheni hii ni pamoja na matoleo mapya ya NOTE 12 series yani NOTE 12 na NOTE 12 VIP ni simu zenye teknolojia ya hali ya juu kuzidi simu ya kampuni nyengine yoyote ya simu yenye kuuzwa kwa sh.800,000, Infinix NOTE Series  zinabaki kuwa kinara zaidi sokoni kutokana na sifa hizi; bei rafiki, kujaa chaji hadi asilimia 100 kwa dakika 17 tu ilihali battery yake inauwezo wa kudumu na chaji kwa siku moja na zaidi, kamera ya Magepixel 108 yenye uwezo wa kuzoom vitu kwa ukaribu na kurecord video za qualiti ya hali ya juu pasipo kusahau Processor ya Mediatek Helio G96 isiyoshindwa kuchezesha game ya aina yoyote na yenye kuchakata kazi za kiofisi kama tu computer”. 

Simu nyengine ambazo zitakuwa katika promosheni ya “KALIKULIKO2022” ni Infinix HOT 12, HOT 12i, HOT 12 play, Infinix Smart 6 na Smart 6+ nunua uzawadie papo hapo lakini pia haitoshi nunua kwa punguzo la kujipangia. Nunua Infinix msimu huu ujionee ukarimu wa kampuni hii kwa wateja wake pasipo kusahau katika mtandao wa kijamii @infinixmobiltz kila wiki NOTE 12 VIP moja itaenda kwa mshiriki bora wa online challenge.

SOMA NA HII  TULISEMA NA IMETOKEA....KUELEKEA MSIMU UJAO..KAPAMA NI MNYAMA...VYUMA VINGINE VINAVYOSUBIRIWA NI HIVI...