Home Habari za michezo INONGA ‘KUIBUKIA’ AL AHALY….ISHU NZIMA IMEKAA HIVI….

INONGA ‘KUIBUKIA’ AL AHALY….ISHU NZIMA IMEKAA HIVI….

Habari za Simba

Inaelelezwa kuwa, Kuna uwezekano mkubwa kwenye mchezo ujao wa Simba SC dhidi ya AI Ahly ya Misri, Beki wa kimataifa raia wa DR Congo, Henock Inonga akaliongoza jahazi la ulinzi baada ya kuanza mazoezi na wenzake.

Takribani majuma mawili Inonga alikuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha aliyoyapata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, dhidi ya Coastal Union baada ya kuchezewa rafu na Hija Ugando na kumfanya kuukosa mchezo wa marudiano dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kuna uwezekano mkubwa sasa wa Inonga kuwa sehemu ya mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Ahly baada ya kuanza mazoezi na wenzake.

“Majeraha ya Inonga yanaelekea kupona kwani tayari vidonda alivyopata vimekauka na kwamba ameanza mazoezi na wenzake jambo ambalo linatupa faraja ya kuamini kuwa atakuwepo kwenye michezo ijayo.

“Tulimkosa Inonga kwenye mchezo uliopita jambo ambalo kwetu lilikuwa gumu ila tunamshukuru sasa amerejea na nafasi yake itaenda kuzibwa bila shaka yoyote hasa baada ya kuanza mazoezi,” amesema Ahmed Ally

SOMA NA HII  KISA KUKOSEKANA KWA DIARA YANGA...MSHERY AWEKA REKODI HII YA KIBABBE CAF...MAMBO YAANZA KUWA MAZURI KWAKE...