Home news BAADA YA KUIBANJUA SIMBA KIMOJA KAVU…MBEYA CITY WAIBUKA NA KUTAMBA NA HILI..

BAADA YA KUIBANJUA SIMBA KIMOJA KAVU…MBEYA CITY WAIBUKA NA KUTAMBA NA HILI..


BAADA ya kufanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo uliopigwa juzi Jumatatu katika Dimba la Sokoine, Mbeya, kocha mkuu wa timu ya Mbeya City, Mathias Lule amefunguka kuwa walijiandaa kucheza pungufu dhidi ya Simba kutokana na rekodi ya timu hiyo kwenye mechi za Ligi Kuu Bara msimu huu.

Mbeya City imekuwa timu ya kwanza kuifunga Simba kwenye ligi msimu huu huku timu hiyo ikiwa miongoni mwa timu zenye mwenendo mzuri wakipoteza mchezo mmoja kati 12 waliyoshuka dimbani, kwa sasa wako nafasi ya tatu kwenye msimamo.

Beki wa Mbeya City, Mpoki Mwakinyuke alitolewa dakika 24 baada ya kupata kadi pili ya njano na kuzaa nyekundu kufuatia kumfanyia faulo Chris Mugalu.

Akizungumza na gazeti la Championi Jumatano, Lule alifunguka kwamba: “Tulijiandaa kwa zaidi ya wiki mbili kuwakabili Simba tulijua watakuja na morali ya ushindi waliyoipata kwenye michuano ya Mapinduzi, hivyo tulipaswa kuwa na tahadhari kubwa kuweza kuwadhibiti.

“Nawapongeza vijana wangu kwa kujituma kwa dakika zote tisini, tulijiandaa kucheza pungufu dhidi ya Simba kutokanana rekodi yao kwenye mechi kadhaa za ligi ambapo baadhi ya timu walizocheza nazo zilipata kadi nyekundu hivyo na sisi tulijiandaa kwa hilo ndiyo sababu kubwa tulifanikiwa kuwadhibiti licha ya kuwa pungufu kwa kipindi kirefu.

SOMA NA HII  KLABU HII LIGI KUU YAANGAMIA...HALI NI TETE MAAJABU PEKEE NDIO YATAIKOMBOA...ISHU NZIMA IPO HIVI