Home Habari za michezo PAMOJA NA KILIO CHA MAMA AKE…TFF WATUPILIA MBALI SHAURI LA FEI TOTO…YANGA...

PAMOJA NA KILIO CHA MAMA AKE…TFF WATUPILIA MBALI SHAURI LA FEI TOTO…YANGA WACHEEKAA…

Habari za Yanga

Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana leo tarehe 2 Machi, 2023 kwa ajili ya kusikiliza pamoja na mambo mengine shauri la mapitio (Review) ya uamuzi wake wa tarehe 9 Januari 2023 kati ya Feisal Salumu na Klabu ya Yanga kama yalivyowasilishwa na muombaji Feisal Salum dhidi ya Klabu ya Yanga

Baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili Kamati imeona kuwa shauri hilo la mapitio (Review) halina msingi wa kisheria kushawishi Kamati kubadili maamuzi yake yaliyotolewa awali na hivyo imetupilia mbali shauri hilo.

Sababu kwa undani za uamuzi huo zitatolewa kwa pande zote mbili zinazohusika katika shauri hilo siku ya Jumatatu 6 Machi, 2023.

Taarifa kamili ya TFF insomeka kama ifuatavyo.

Habari za Yanga

SOMA NA HII  YANGA WASHINDWE WENYEWE AISEE...CAF WAIPA URAHISI WA KUBEBA UBINGWA WA SHIRIKISHO...