Home Tetesi za usajili MSHAMBULIAJI ALIYEKUWA KWENYE RADA ZA YANGA KUIBUKIA SIMBA

MSHAMBULIAJI ALIYEKUWA KWENYE RADA ZA YANGA KUIBUKIA SIMBA


 IMEELEZWA kuwa mabosi wa Simba wapo kwenye mazungumzo ya mwisho kukamilisha dili la mshambuliaji wa Mbeya City, Kibu Denis.

Mshambuliaji huyo alikuwa anatajwa pia kuwa kwenye rada za Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi na ilikuwa inatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la nyota huyo.

Ndani ya Mbeya City nyota huyo ametupia abao 7 na ametoa pasi tatu za mabao hivyo akikamilisha dili lake la kujiunga na Simba ana kazi ya kupambana kupenya kikosi cha kwanza kwa kuwa atakutana na washambuliaji wenye ushkaji mkubwa na nyavu.

Uwepo wa John Bocco mwenye mabao 16, Meddie Kagere mwenye mabao 13 na Chris Mugalu mwenye mabao 15 kutamfanya awe na kazi ya kuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Didier Gomes.

 Hivi karibuni, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara aliweka wazi kwamba wamekamilisha usajili wa nyota watatu ambao watatambulishwa hivi karibuni.

SOMA NA HII  WAKATI LA CHAMA LIKIWA LA MOTO....NTIBAZONKIZA NAYE AWAVIMBIA MABOSI SIMBA...ISHU HII HAPA...