Home Simba SC MZEE WA KUKERA MORRISON KUIWAHI YANGA KIGOMA

MZEE WA KUKERA MORRISON KUIWAHI YANGA KIGOMA


 MZEE wa kukera ndani ya uwanja, Bernard Morrison kwa sasa amesharejaea ndani ya ardhi ya Tanzania baada ya kutokuwepo kwa muda kutokana na matatizo ya kifamilia.

Nyota huyo ambaye mabosi wa Azam FC hawana hamu naye kutokana na kitendo chake cha kuanzisha faulo harakahara kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ulikuwa ni nusu fainali huenda atakuwa kwenye kikosi kitakachoivaa Yanga.

Pia kipa namba moja wa Namungo FC, Jonathan Nahimana naye hana hamu naye kwa kuwa alimtungua bao akiwa nje ya 18 kwenye mchezo wa ligi jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Namungo kuyeyusha pointi tatu mazima kwa kufungwa mabao 3-1.

Mtu wa karibu wa Morrison amesema kuwa nyota huyo tayari amerudi Dar tayari kwa ajili ya mchezo ujao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga.

“Tayari Morrison yupo Dar na hivyo anaweza kuwa kwenye kikosi kitakachoanza dhidi ya Yanga ikiwa mwalimu atahitaji,” ilieleza taarifa hiyo.

Hivi karibuni, Kocha Msaidizi wa Simba, Seleman Matola aliweka wazi kwamba Morrison atarejea kikosini hivi karibuni.

“Morrison atarejea kikosini hivi karibuni kwa kuwa alikuwa kwenye matatizo ya kifamilia, alikuwa kwao nchini Ghana,” .

Kwenye mchezo wa ligi wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa, Julai 3 ukisoma Simba 0-1 Yanga aliyeyusha dk 90.

Wanatarajiwa kukutana tena Kigoma, Julai 25 kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA HUYU HAPA...KASHINDA LIGI YA MABINGWA NA TP MAZEMBE..KOCHA WA BILION 1.17 APIGWA CHINI