Home Habari za michezo HUU HAPA USAJILI MPYA YANGA …ENG HERSI AUNGANISHIWA DILI AKIWA PSG….

HUU HAPA USAJILI MPYA YANGA …ENG HERSI AUNGANISHIWA DILI AKIWA PSG….

Habari za Yanga

IMEFICHUKA kuwa, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ameenda Ulaya akiwa na hesabu za kukamilisha usajili wa kushtua iwapo atafanikiwa kumnasa straika anayecheza soka barani humo.

Yanga imebakiza mastaa wawili tu wa kuongeza kikosini akiwamo winga wa maana wa kulia huku hesabu zao zikiwa kwa Agee Basiala wa Union Maniema ya DR Congo ambaye tayari ameshatumiwa mkataba wa miaka miwili.

Hesabu za Yanga zilizosalia ni kufanya usajili wa mshambuliaji wa kati mwenye ubora na hapo ndipo ikafahamika kwamba Hersi atashuka na mtu.

Hersi alikuwa Ufaransa kwa ziara ya mualiko na mabosi wa klabu kubwa ya Paris Saint German (PSG) lakini ndani yake kuna hesabu za usajili.

Inaelezwa Hersi atakutana na viongozi wa klabu moja ya Asia waliopo Ufaransa kuangalia uwezekano wa kumnasa mshambuliaji mmoja.

Yanga inataka kuwa na mshambuliaji ambaye atawasaidia sasa kwenye msimu huu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tunahitaji mshambuliaji wa kati na na kuhakikishia Hersi hatarudi patupu, atashuka na mshambuliaji wa maana wa kuipa ubora timu,” alisema bosi wa juu wa Yanga.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUWA NA KESI YA KUJIBU DHIDI YA KARIA....MANARA AIBUKA NA MAMBO YA SLOGAN...ATAKA SERIKALI IINGILIE KATI..