Home Habari za michezo PAMOJA NA KUSAJILIWA NA WAARABU JUZI JUZI…..RONALDO AJIRUDISHA MADRID KIAINA…

PAMOJA NA KUSAJILIWA NA WAARABU JUZI JUZI…..RONALDO AJIRUDISHA MADRID KIAINA…

Staa wa klabu ya Al Nassr Cristiano Ronaldo ameitembelea klabu ya Real Madrid inayoshiriki michuano ya Spanish Super Cup inayofanyika nchini Dubai.

Ronaldo ameonekana kwenye uwanja wa mazoezi ambao unatumiwa na Real Madrid jijini Riyadh nchini Saudia kujiandaa na fainali ya mchezo wa Spanish Super Cup dhidi ya Barcelona utakaopigwa siku ya Jumapili nchini humo.

Staa huyo ameonesha bado ana uhusiano mzuri na klabu ya Real Madrid ambayo aliitumikia kwa takribani miaka tisa na kuacha rekodi za kutisha ndani ya klabu hiyo kubwa kabisa ulimwenguni.

Ronaldo aliondoka ndani ya klabu ya Real Madrid akiwa kama mfungaji bora wa muda wote wa timu hiyo huku akiisaidia klabu hiyo kutwaa mataji ya kutosha.

SOMA NA HII  BAADA YA KUIONA SIMBA IKIPATA USHINDI WA TAABU JANA...'TRY AGAIN' ASHINDWA KUJIZUIA..ATOA TAMKO JIPYA..