Home news SIMBA YATUMA MAJINA 31 CAF..CHIKWENDE ATEMWA..WAONGEZA VIFAA VIPYA VIWILI KIMYAKIMYA…

SIMBA YATUMA MAJINA 31 CAF..CHIKWENDE ATEMWA..WAONGEZA VIFAA VIPYA VIWILI KIMYAKIMYA…


Wakati Yanga wakiwasilisha jeshi la wachezaji 28 watakaocheza mechi za kimataifa CAF,  watani wao Simba wakaongeza wachezaji watatu tu zaidi yao wakipeleka mastaa 31 tayari kwa mashindano hayo ambapo nao wakapeleka mastraika 6 tu.

Simba imepeleka makipa wanne ambao ni chaguo lao la kwanza Aishi Manula, Benno Kakolanya, Jeremiah Kisubi na Ally Salim katika orodha hiyo.

Safu ya ulinzi ina mabeki tisa ambao ni; Erasto Nyoni, Mohammed Hussein, Gadiel Michael, Henock Inonga ‘Varane’, Israel Mwenda, Joash Onyango, Pascal Wawa, Kennedy Juma na Shomari Kapombe, huku eneo la kiungo likiwa na watu 12 ambao ni Abdulswamad Kassim, Bernard Morrison, Duncan Nyoni, Hassan Dilunga, Jimmyson Mwanuke, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na Pape Ousmane Sakho.

Wengine ni Peter Banda, Rally Bwalya, Sadio Kanoute na Thadeo Lwanga, huku kwenye ushambuliaji kuna nahodha John Bocco, Meddie Kagere, Chriss Mugalu, Yusuph Mhilu, Ibrahim Ajibu na Kibu Denis.

Simba ambao wataanzia hatua ya kwanza wao kama watafanikiwa kutinga hatua ya makundi watapata nafasi ya kuongeza idadi ya wachezaji 9 pekee ili kukidhi kanuni ya wachezaji 40 ambao wanahitajika.

SOMA NA HII  KWA MUJIBU WA KANUNI SASA MAMLAKA ZITANGAZE RASMI YANGA IMESHUKA DARAJA...

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here