Home Habari za michezo WAKATI MASHABIKI WAKINGOJA KIUNGO MKABAJI MPYA….KOCHA SIMBA AIBUKA NA HILI JINGINE TENA...

WAKATI MASHABIKI WAKINGOJA KIUNGO MKABAJI MPYA….KOCHA SIMBA AIBUKA NA HILI JINGINE TENA KUHUSU KANOUTE….


Achana na maufundi ya Mwamba wa Lusaka, Clatous Chama ambaye amekuwa gumzo na hata Pape Sakho na Peter Banda, Sadio Kanoute ni habari nyingine hiyo ni kwa mujibu wa maneno ya kocha wa Simba, Zoran Maki.

Licha ya kwamba Kanoute hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kilienda Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu huu wa 2022/23 siku chache za mazoezi aliyofanya jijini hapa zilitosha kumkuna kocha huyo.

Kanoute alianza kuula kwenye mchezo wa kirafiki kwenye kilele cha Simba Day dhidi ya St. George ya Ethiopia ambapo alicheza sambamba na Jonas Mkude kama viungo wakabaji pacha na kuisaidia timu yao kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Tangu hapo amekuwa akipata shavu kwenye michezo mfululizo zaidi kwenye mchezo ulioputa wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar alitumika mwenyewe eneo la kiungo mkabaji na kuupiga mwingi.

Kwanini Zoran aliamua kumchezesha peke yake? katika mahojiano maalumu na gazeti hili alisema, “Nilihitaji kuwa na idadi kubwa ya viungo wenye sifa ya kushambulia ili tutengeneze zaidi nafasi za mabao kwenye hilo tulifanikiwa,”

“Kama uliona vizuri tangu mchezo wetu wa kwanza wa msimu kuna mabadiliko niliyafanya yalilenga hicho, niliona Kanoute peke yake anatosha kuweka uwiano mzuri kwenye kujilinda.”

Kocha huyo aliendelea kuongea kwa kusema anafurahishwa na uchezaji wa Kanoute, “Ni kati ya wachezaji ambao ni wepesi kushika na kufanyia kazi maelekezo,”

“Kuhusu uwezekano wa kuanza na kiungo mkabaji mmoja au wawili itakuwa inategemea na mahitaji ya timu kulingana na mchezo ambao utakuwa mbele yetu,” alisema Zoran.

SOMA NA HII  BALOZI WA UINGEREZA ALIVYOWAPA MAUJANJA SIMBA LEO...AHADI YAKE KUBWA NI HII HAPA...