Home Uncategorized Kwanini tunasita kumwiita Manula , Tanzania one?

Kwanini tunasita kumwiita Manula , Tanzania one?

Wakati niko shule msingi nilikuwa najaradia madaftari yangu kwa magazeti ya michezo. Nilikuwa mteja mkubwa sana wa magazeti haya. Nilipenda kuyasoma, nilikuwa nafanya kila niwezalo ili nipate pesa ya kununua magazeti haya ili nisome tu.

Hii ndiyo ilikuwa moja ya furaha yangu. Niliiba hela nyumbani ili nikanunue magazeti ya michezo tu. Hata wanafunzi wenzangu walikuwa wanajua ni wapi pakuyapatia magazeti yangu. Unataka kusoma habari za michezo ? Mfuate Kiyumbi hawezi kosa magazeti ya michezo. Ndicho kipindi ambacho nilikuwa na idadi kubwa ya magazeti ndani. Na ndicho kipindi ambacho nilikuwa nayafunika madaftari yangu kwa magazeti haya. Kilikuwa kitu cha kawaida sana kwangu.

Kwenye magazeti mengi ambayo nilikuwa nayajaradia kwenye madaftari yangu kulikuwa na habari ambayo ilikuwa inamhusisha Juma Kaseja. Habari ambayo ilikuwa na nakshi kwa mbele kwa neno “Tanzania One” . Hii ndiyo nakshi ambayo ilikuwa inakaa mbele ya jina lake kwenye kila gazeti.

Kuna wakati jina lake lilifunikwa na jina la Tanzania One. Yani ilionekana neno Tanzania One lilistahili kuwa jina lake kabisa halisi. Na hii ni kutokana na kiwango kikubwa ambacho alikionesha Juma Kaseja kipindi kile. Ikaonekana hakuna golikipa ambaye anaweza kumpa changamoto.

Ilikuwa ngumu kumuondoa pale kwenye nafasi yake ya golikipa wa kwanza wa timu ya taifa. Ungemweka nani mbele ya Juma Kaseja?

Ilikuwa ngumu sana kumuondoa eneo lile mpaka pale Maximo alipoamua kutumia kiburi kumweka Ivo Mapunda kwa sababu ya umbo lake tu refu.

Muda mrefu umepita tangu Juma Kaseja asiwe mmoja wa wachezaji wa timu ya taifa. Leo hii Tanzania inamshuhudia Aishi Manula kama golikipa namba` moja wa timu ya taifa.

Lakini mpaka sasa hivi vyombo vya habari, watu hawamtambui kama Tanzania one, hapa ndipo linapokuja swali kwanini mpaka sasa hivi Tanzania haitaki kumtambua Manula kama Tanzania one ???

The post Kwanini tunasita kumwiita Manula , Tanzania one? appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  UONGOZI YANGA WATOA TAMKO JUU YA UJIO WA JAMES KOTEI