Home Uncategorized STARS KUOGELEA MIZAWADI KIBAO AFCON

STARS KUOGELEA MIZAWADI KIBAO AFCON


Michuano ya Afcon ambayo inatarajiwa kuanza Juni 21 nchini Misri sio ya kitoto kwani bingwa wa michuano hiyo analamba mkwanja mrefu.

Tanzania inapeperusha Bendera kwenye michuano hii ikiwa kundi C ambalo lina timu nyingine ambazo ni Senegal, Kenya na Algeria na mchezo wa kwanza kwa Tanzania utakuwa Juni 23 dhidi ya Senegal.

Hivyo endapo atatwaa ubingwa itogelea mizawadi
Zawadi za michuano hiyo zipo namna hii:

BINGWA wa michuano ya Afcon anapewa zawadi ya dola milioni 4.5 sawa na bilioni 10.

Mshindi wa pili anapewa dola milioni 2.5 sawa na bilioni 5.7.

Mshindi wa tatu analamba dola milioni 2.0 sawa na bilioni 4.6.

Timu itakayotinga robo fainali inapewa dola 800,000 sawa na bilioni 1.8.

SOMA NA HII  SOMO LA KATUMBI KWA MO DEWJI JUU YA UWEKEZAJI