Home Uncategorized KABLA YA JUNI 30 MRITHI WA NDAYIRAGIJE KUJULIKANA

KABLA YA JUNI 30 MRITHI WA NDAYIRAGIJE KUJULIKANA


UONGOZI wa KMC umesema kuwa kwa sasa unaendelea na mchakato wa kumtafuta Kocha Mkuu atakayebeba mikoba ya Etienne Ndayiragije aliyetimkia Azam FC.

Akizungumza na Salehe Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Anwari Binde amesema kuwa kwa sasa michakato inaendelea ambapo tayari wameshawafanyia usaili makocha wengi wakubwa.

“Tunafanya usaili kwa umakini ili kumpata kocha atakayebeba mikoba ya mwalimu wetu ambaye ameondoka ,hivyo hatutakurupuka kumpata kocha mpya.

“Wengi wameleta CV zao na zimepitiwa ambapo kwa yule atakayekidhi vigezo atapewa mkataba, kabla ya Juni 30 nina imani tutakuwa tumempata mwalimu,” amesema Binde.

SOMA NA HII  TAMBWE AMEMTUMIA UJUMBE HUU ZAHERA KUHUSIANA NA YONDANI