Home Habari za michezo KWA MKAPA KUMEDODA…MECHI SIMBA NA YANGA MASHABIKI HAKUNA…ISHU NZIMA IKO HIVI

KWA MKAPA KUMEDODA…MECHI SIMBA NA YANGA MASHABIKI HAKUNA…ISHU NZIMA IKO HIVI

KWA MKAPA KUMEDODA...MECHI SIMBA NA YANGA MASHABIKI HAKUNA...ISHU NZIMA IKO HIVI

Zikiwa zimebaki saa Chache kuanza kwa mtanange wa Simba na Yanga hali inaonekana kupoa nje ya Uwanja wa Benjamin Mkapa tofauti na ilivyozoeleka kwenye derby zilizopita.

Mchezo huo unaozikutanisha timu vigogo za Tanzania zenye mashabiki wengi unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 11:00 jioni lakini hadi sasa shamrashamra nje ya uwanja zimeonekana kuwa chache.

Pamoja na kupoa, lakini biashara nyingine ndogondogo zimeonekana kuendelea huku mashabiki wakiendelea kufika eneo la tukio japo kwa uchache.

Hali ya hewa ipo shwari hadi sasa na maofisa mbalimbali wa ulinzi wakiwemo Polisi wapo pia nje na ndani ya uwanja wakiendelea kuhakikisha amani na ustaarabu.

Aidha kuna baadhi ya maeneo yameonekana kuendelea kuuza tiketi za kuingia uwanjani huku kukiwa na misongamano kwa makundi.

SOMA NA HII  MECHI YA YANGA YAAHIRISHWA