Home Habari za michezo KISA KUMFUNGA MAZEMBE DAR…YANGA WATABIRIWA KUTINGA FAINAL YA SHIRIKISHO AFRIKA..

KISA KUMFUNGA MAZEMBE DAR…YANGA WATABIRIWA KUTINGA FAINAL YA SHIRIKISHO AFRIKA..

Habari za Yanga

Mwamuzi mwandamizi wa soka nchini Tanzania, Osman Kazi amewatabiria makubwa Timu ya Yanga akisema kuwa kutokana na kiwango walichokionyesha kwa siku za hivi karibuni hususan mchezo wao dhidi ya TP Mazembe ana uhakika timu hiyo inaweza kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kazi amesema hayo jana wakati akihojiwa na wanahabari kutoa tathmini yake mara baada ya mchezo wa Kundi D wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika kumalizika huku Yanga akiibuka na ushindi mnono wa bao 3-1 dhidi ya Mazembe.

“Nyota wa mchezo kwa Yanga ilikuwa ni timu nzima, kulikuwa na ari kubwa ya kujituma kuanzia kwa Diarra mpaka mchezaji wa mwisho, wote wameota mchango unaostahili. Tofauti na mechi ya Simba na Raja, leo nimeona pumzi ya moto ikipelekwa haswa, Yanga wameupiga mwingi mno.

“Kwa kiwango ambacho  wamekionyesha leo, usishangae kuwaona  wakicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Kiwango chao kilikuwa ‘supab’, ‘exellent’ niwape ‘big up’ walistahili kwa kile walichokivuna, binafsi sina shaka na Yanga,” amesema Othman.

SOMA NA HII  TAMBWE:BADO SIJALIPWA BADO NA YANGA