Home Habari za michezo BAADA YA KIMYA KIREFU…BARBARA AANZA KWA KUIPONGEZA YANGA…HUENDA YA SENZO YAKAJIRUDIA..?

BAADA YA KIMYA KIREFU…BARBARA AANZA KWA KUIPONGEZA YANGA…HUENDA YA SENZO YAKAJIRUDIA..?

Habari za Michezo

Aliyekuwa C.E.O wa Simba Barbara Gonzalez amewapongeza Yanga kwa kuibuka na ushindi ya goli tatu dhidi ya TP Mazembe na kupokea kiasi cha Tsh Milioni 15 kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan na kuongeza kuwa walistahili hayo kutokana na kuwa bora.

Barbara amesema hayo jana Jumapili, Februari 19, 2023 wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya mchezo wa yanga dhidi ya TP Mazembe ya Congo DR ambapo Yanga aliibuka na ushindi wa bao 3-1.

Kumekuwa na mitazamo tofuati kuwa huenda Mwanadada huyo ambaye hivi karibuni alitimiza miaka 33 akafuata nyendo za Senzo za kuhamia upande wa pili, kitu ambacho hata hivyo ni asilimia 0 kati ya 100 kwani mbali na kuwa mtumishi wa Simba wakati ule, pia alikuwa ni mtu wa karibu sana na Mo Dewji.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Kennedy Musonda dakika ya 7, Mudathiri Yahya dakika ya 11 na Tuisila Kisinda dakika ya 90+2’ wakati bao la kufutia machozi kwa Mazembe likifungwa na Alex Ngonga dakika ya 80.

Mbali na alama 3, Yanga inaondoka uwanjani na uhakika wa milioni 15 kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan na milioni 3 kutoka kwa uongozi wa Mkoa wa Mtwara.

Matokeo mengine;
Yanga SC 3-1 TP Mazembe
Lupopo 1-2 Marumo
Bamako 1-1 US Monastir
Rivers Utd 3-0 ASEC Mimosas
Future 1-1 Pyramids
Al Akhdar 1-1 USM Alger
AS FAR 5-1 Kara
DCMP 0-0 Diables Noirs.

SOMA NA HII  FT: COASTAL UNION 0-2 YANGA SC...MAYELE KAMA KAWA AENDELEZA ALIPOISHIA...MORRISON AANZA KUWAKERAAAH....