Home Habari za michezo KISA KIPIGO KUTOKA KWA WAMOROCCO…MO DEWJI AIBUKA NA ‘KAULI HII YA KIBABE’...

KISA KIPIGO KUTOKA KWA WAMOROCCO…MO DEWJI AIBUKA NA ‘KAULI HII YA KIBABE’ SIMBA…

Habari za Simba

Rais wa heshima wa Klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji ‘MO’ amewaambia mashabiki wenzake wa klabu hiyo kwamba wasikate tamaa licha ya kupoeteza dhidi ya Raja Casablanca wikiendi iliyopita.

MO amesema, mashabiki wa kweli huwa wanakuwa pamoja na timu kwenye nyakati zote, ziwe nzuri au mbaya.

“Simba, tunashinda pamoja, tunafungwa pamoja. Hatu kati tamaa. Tutaendeleza mapambano!,” Mo Dewji Muwekezaji wa Klabu ya Simba SC.

Simba anatarajia kushuka dimbani tena leo kwenye Ligi Kuu ya NBC ambapo atavaana na Wanalambalamba wa Azam FC kisha atafunga safari kwenda Uganda kuwafata Vipers mechi ya Klabu Bingwa itakayochezwa Jumamosi Februari 25, 2023.

SOMA NA HII  PAMOJA NA WOTE KUWA MISRI....SIMBA WAIPOTEZEA KIMTINDO AZAM FC...WADAI HAWANA 'TIME' NAO..KILA MTU AFE KIVYAKE...