Home Uncategorized NIYONZIMA,TSHISHIMBI NA MARRISON WAWEKWA MTEGONI YANGA..!!

NIYONZIMA,TSHISHIMBI NA MARRISON WAWEKWA MTEGONI YANGA..!!

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa amewawekea mtego mastaa wa timu hiyo kwa kuwaambia kuwa ukweli wa nani alikuwa anafuata kwa usahihi program za mazoezi ambazo wamewaachia katika kipindi cha mapumziko utajulikana mara baada ya kukutana na atakayekutwa anategea, basi adhabu kubwa itampata ikiwemo kukatwaa mshahara.

 Benchi la ufundi la timu hiyo chini ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Luc Eymael waliwapa program hizo wachezaji wote ambayo kila mmoja inamuagiza afanye mazoezi ya aina gani wakati wa kipindi hiki Ligi Kuu Bara imesimama ikipisha Virusi vya Corona.

 Tayari baadhi ya wachezaji wameonekana wakifanya mazoezi kupitia mitandao ya kijamii ambao ni Bernard Morrison, Haruna Niyonzima, Papy Tshishimbi, Metacha Mnata, Juma Abdul na Ally Mtoni ‘Sonso’.

Akizungumza na gazeti la Championi Jumamosi, Mkwasa alisema kuwa wamepokea video za wachezaji wote kwa kupitia WhatsApp zikiwaonyesha wakifanya mazoezi, hivyo ngumu kuamini kama kweli wanafanya kwa ufanisi huku wakipanga kujiridisha baada ya kukutana kuanza mazoezi ya pamoja.

“Mara baada ya Serikali kusitisha michezo na mikusanyiko kwa siku 30 kuzuia kuenea kwa Virusi vya Corona, benchi letu la ufundi lilitoa programu za mazoezi kwa kila mchezaji wetu.“Baada ya kutoa program hiyo, kocha Eymael aliwataka kuwatumia makocha wote video kila wiki na ratiba hiyo ilikuwa ya mazoezi binafsi kwa kila mchezaji akiwa nyumbani kwake.

 “Ni vigumu kumfuatilia mchezaji na kumsimamia kufanya mazoezi akiwa kwake, lakini mchezaji mwenyewe anapaswa kutambua majukumu yake na kutekeleza kwa kuwa hiyo ni kazi yake ambayo anaitegemea kupata kipato, kila kitu kitajulikana baada ya kuanza mazoezi ya pamoja nani alikuwa anategea na nani alikuwa anafuata program kwa usahihi,” alisema Mkwasa.

SOMA NA HII  PATA BONASI MPAKA YA 80000/ KUTOKA MERIDIAN BET SASA