Home Uncategorized PAMOJA NA KIWANGO KIKUBWA..STARS YABAKI PALEPALE FIFA

PAMOJA NA KIWANGO KIKUBWA..STARS YABAKI PALEPALE FIFA

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeendelea kubaki nafasi ya 134 kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) vya mwezi Machi 2020.

Kufutwa kwa ratiba ya mechi za kimataifa ambazo zilipangwa kuchezwa mwezi huo kutokana na kasi ya maambukizi ya virusi vya corona, kunaonekana kuiathiri Stars ambayo imejikuta ikibaki na pointi 1086 ilizokuwanazo mwezi Februari.

Hilo halijatokea kwa Stars tu bali nchi zote wanachama wa FIFA zimeendelea kubakia nafasi zao za awali pasipo kuongezeka au kupungua kwa pointi kama zilizokuwa nazo katika viwango vya mwezi uliopita.

Uganda imeendelea kuwa kinara kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwa nafasi ya 77 ikifuatiwa na Kenya iliyo nafasi ya 107 kidunia huku ikishika nafasi ya 128.

Nchi nyingine zilizo ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na nafasi zao kwenye mabano ni Rwanda (131), Ethiopia (146), Burundi (149), Sudan Kusini (168), Djibout (184), Somalia (196) na Eritrea (205).

Kiujumla Ubelgiji inaongoza ikifuatiwa na Ufaransa, nafasi ya tatu wako Brazil, England wanashika nafasi ya nne wakati Uruguay wako nafasi ya tano.

Kwa Afrika, vinara ni Senegal wakifuatiwa na Tunisia na nyuma yao wapo Nigeria wakati wanaoshika nafasi ya nne ni Morocco na Ghana wako nafasi ya tano huku kidunia wakiwa nafasi ya 46.

SOMA NA HII  KISA CORONA...SHIBOUB ASUBIRI RUHUSA YA RAIS SUDANI KURUDI TZ..!!