Home Habari za michezo KOCHA YANGA AMWAGA SIRI NZITO…ATATUMIA MBINU HIZI KUWAANGAMIZA RIVERS

KOCHA YANGA AMWAGA SIRI NZITO…ATATUMIA MBINU HIZI KUWAANGAMIZA RIVERS

KOCHA YANGA AMWAGA SIRI NZITO...ATATUMIA MBINU HIZI KUWAANGAMIZA RIVERS

Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Mohammed Nabi amesema kuwa katika mchezo wa kesho dhidi ya Rivers United, hatapaki basi badala yake atashambulia na kujilinda kwa tahadhari ili asiruhusu timu yake kufungwa.

“Nabi amesema hayo leo Jumamosi, Aprili 29, 2023 wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelekea mchezo wao wa marudiano wa robo fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United ya Nigeria.

“Mchezo tutau-balance, tutacheza kuzuia tusifungwe goli na tutashambulia ili tupate goli, kwa hiyo mchezo utakuwa wa namna hiyo.

“Nikisema nianike kila kitu kwa undani nitakuwa kama nauza mbinu zangu kwa mshindani wangu siku moja kabla ya mechi. Kifupi ni kwamba tutazuia na kushambulia kwa pamoja,” amesema Nabi.

Yanga wakiwa na mtaji wa bao 2-0, kesho watashuka katika dimba la Mkapa kukipiga na Rivers United wakisaka tiketi ya kusonga katika hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika.

SOMA NA HII  MOLINGA: CHAMA HAPATI NAMBA YANGA...NI MUDA SAHIHI