Home Habari za michezo HUYU BWANA KAMA ANATAKA KUFANIKIWA BASI AONDOKE YANGA

HUYU BWANA KAMA ANATAKA KUFANIKIWA BASI AONDOKE YANGA

Mshery golikipa wa Yanga

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia Wasafi Media, Nasir Khalfan amesema kuwa kipa namba tatu wa Yanga, Aboutwalib Mshery anapaswa aondoke kwenye klabu hiyo ili akapate changamoto kwani amekuwa hapati nafasi ya kudaka licha ya kuwa kipa mzuri.

Nasri kupitia Wasafi FM amesema hayo wakati akizungumzia kuhusu tatizo alilolisema kocha wa Taifa Stars Adel Amrouche kwamba taifa linakosa makipa wazawa wenye ubora wa kuipambania timu ya taifa.

Nasir amesema kuwa anaamini kuna makipa wazuri wengi vijana nchini ambao kama wangepata nafasi na makocha wazuri wa makipa, basi wangeweza kufanya vizuri na kufika mbali.

“Kipa kama Mshery wa Yanga, inawezekana ushindani wa namba umemshinda lakini binafsi ninaamini angepitishwa njia sahihi basi angekuwa kipa mzuri sana kwa taifa letu.

“Mfano mzuri Novatus Miroshi hakufanya vizuri Azam FC sababu ya ubora wa wachezaji waliokuwepo pale ikawa ngumu kwake kufanikiwa lakini alipopelekwa kwa mkopo na sasa yupo Shakter Donetsk.

“Wasimamizi wake walifanya kazi yao vizuri wakaona ni ngumu kwake kufanya vizuri Azam FC wakampeleka kwa mkopo na hapo ndipo alipofanikiwa.

“Ni kweli ushindani wa nafasi kwa Mshery mbele ya Diarra pale Yanga ni mkubwa na ngumu kwake kufanikiwa lakini wasimamizi wake wanaweza kufanya kazi nzuri ya kumtoa pale na kumpeleka sehemu nyingine atakapopata nafasi ya kucheza na kufanikiwa zaidi ya hapa alipo,” amesema Nasir Khalfan.

SOMA NA HII  MWAMBA HUYU HAPA KUTOKA CHIPOLOPOLO AIUNGA MKONO POWER DYNAMO DHIDI YA SIMBA