Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA KESHO SIMBA vs AL AHLY…JEMEDARI SAID ATUPA KOMBORA HILI...

KUELEKEA MECHI YA KESHO SIMBA vs AL AHLY…JEMEDARI SAID ATUPA KOMBORA HILI KWA YANGA…

Habari za Simba na Yanga

Mchambuzi wa masuala ya soka nchini, Jemedari Said Bin Kazumari amesema kuwa Klabu ya Simba imewaacha mbali wapinzani wao Yanga SC kwenye soka la Kimataifa.

Jemedari amesema hayo kuelekea mchezo wa kesho wa African Football League kati ya Simba na AL Ahly, yakiwa ni mashindano mapya ya CAF huku Simba ikitarajiwa kuandika historia ya kuwa timu ya kwanza nchini Tanzania kushiriki michuano hiyo.

“Kwani unadhani Yanga walivyoingia fainali Simba walifurahia. Hata wao hawawezi kufurahia Simba kucheza African Football League na kwa kuwa hawana imani kama Al-Ahly anaweza kushinda dhidi ya Simba hawawezi kwenda uwanjani.

“Zamani walikuwa wanaenda kwa sababu walikuwa na uhakika Simba itafungwa. Kama Ahmed Ally anavyosema mwakani hadi IHEFU watashiriki African Football League, aliyeanza kaanza tu.

“Acheni kufichaficha, Simba ndio imefanya Tanzania iogopwe, waarabu zamani walikuwa wakipangwa na timu za Tanzania wanashangilia lakini kwa sasa hawataki kabisa yote Simba ndio kasababisha.

“(Yanga) Wanasema wamewaacha mbali, mbali hiyo wapi, maana inategemea na unatoka wapi. Simba imewaacha mbali sana kimataifa,” amesema Jemedari Saidi.

SOMA NA HII  KUHUSU UWEZO WA AKPAN..MGUNDA AMALIZA UTATA ...AANIKA WACHEZAJI WANAOSTAHILI SIMBA ...