Home Uncategorized HIZI HAPA SILAHA MATATA ZA MAKOCHA LEO AMBAZO ZIMESHIKILIA USHINDI NELSON MANDELA

HIZI HAPA SILAHA MATATA ZA MAKOCHA LEO AMBAZO ZIMESHIKILIA USHINDI NELSON MANDELA


SIMBA SC inayonolewa na Sven Vandenbroeck leo ina kazi ya kumenyana na Namungo FC inayonolewa na Hitimana Thiery kwenye mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga majira ya saa 9:00 alasiri huku timu zote mbili silaha zao za kazi zikiwa ni kwa upande wa viungo kutengeneza mipango ya ushindi.

Kwa upande wa Simba silaha namba moja ni Clatous Chama kwa upande wa viungo ambapo yeye ni kinara wa
kutengeneza mipango ndani ya Simba kwenye
kombe la Shirikisho na ni namba moja kwa kucheka
na nyavu.

Ana jumla ya pasi tatu za mabao na amefunga
mabao manne ndani ya Kombe la Shirikisho.


Kwa ujumla Chama amekuwa ni nyota kwenye utengenezaji mipango na ndani ya ligi ni kinara pia akiwa na pasi 10 na mabao mawili kwa namna moja ama nyingine silaha ya ushindi ipo kwa nyota huyu.

Lukas Kikoti ni kiungo machachari ndani ya
Namungo ambaye amekuwa akimpa hofu kubwa
Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck
kutokana na uwezo wake ndani ya uwanja.

Kwenye Ligi Kuu Bara ametengeneza jumla ya pasi
saba na kufunga mabao manne na Sven anajua
shughuli yake.

Hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa hasa sehemu ya viungo ambapo kila mwalimu ana mbinu zake za kusaka ushindi.

SOMA NA HII  SURE BOY: WACHEZAJI TUPO TAYARI KWA USHINDANI