Home Habari za michezo SIMBA WAIFANYIA UMAFIA ASEC…MO DEWJI ATUA KAMBINI…RAIS SAMIA AHUSISHWA KWENYE MCHAKATO…

SIMBA WAIFANYIA UMAFIA ASEC…MO DEWJI ATUA KAMBINI…RAIS SAMIA AHUSISHWA KWENYE MCHAKATO…


KLABU ya Simba imeonyesha kutotaka utani baada ya kuweka wazi wana mpango wa kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa katika ardhi ya ugenini.

Simba kesho watakuwa na kibarua dhidi ya ASEC Mimosas nchini Benin na wanahitaji ushindi au pointi ya aina yoyote ili waendelee kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally akiwa nchini Benin, amesema lengo laoni kufuzu hatua ya makundi wakiwa ugenini.

Ahmed amesema tayari walishafuzu mara mbili wakiwa nyumbani (Mkapa) hivyo ni wakati wao kufuzu wakiwa ugenini na hilo linawezekana.

“Tunataka iwe kama zawadi kwa Rais wetu wa nchi kufuzu hatua ya robo fainali tukiwa ugenini, tunajua tutazidi kuitangaza Simba na Tanzania kiujumla,” amesema Ahmed.

Ahmed alifichua siri nyingine akisema Rais wao wa heshima, Mohammed Dewji alipoenda kuwatembelea kambini hivi karibuni aliwaambia anataka kombe.

“Mo alipokuja kambini alisema lengo lake ni kuona Simba ikichukua kombe lolote Afrika  hivyo wachezaji nao wanaishi humo,” alisema Ahmed.

Simba kama ikishinda kwenye mchezo wao wa kesho watafikisha pointi 10 na mchezo wao ujao dhidi ya USGN watamalizia nyumbani katika uwanja wa Mkapa.

Mpaka sasa kundi lilivyo nafasiu ya pili wanashika Asec wakiwa na pointi sita, Berkane wanashika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 6 na nafasi ya nne wa wanashika USGN wakiwa na pointi nne.

Mchezo mwingine utakaopigwa kesho ni USGN dhidi ya Berkane utakaopigwa saa 1:00 usiku.

SOMA NA HII  BAADA YA KUGUNDUA HUENDA MAMBO YAKAENDA KOMBO..PABLO KAAMUA KUJA NA HILI JIPYA MSIMBAZI...