Home Uncategorized KAGERE AAAMKA NA JIPYA SIMBA

KAGERE AAAMKA NA JIPYA SIMBA


Mshambuliaji tegemeo wa Simba Mnyarwanda, Meddie Kagere amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuwa watafanya kila liwezekano wachukue ubingwa wa Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

Kauli hiyo aliitoa mara baada ya timu yao kuondolewa kwenye raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba imeondolewa kwenye raundi hiyo na UD Songo ya Msumbiji baada ya sare ya bao 1-1 hapa nyumbani na ugenini walitoka suluhu hivyo wametolewa kwa faida ya bao la ugenini.

Kagere alisema kuwa anafahamu uchungu walioupata mashabiki ambao nao wachezaji wameupata, hivyo watarajie mengi mazuri.

Kagere alisema kuwa hivi sasa mashabiki waelekeze nguvu na akili kwenye ligi na michuano mingine watakayoshiriki kwa kuchukua mataji yote.

“Wote tumeumia baada ya matokeo mabaya ya kuondolewa na Songo katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Hayakuwa malengo yetu sisi kuondolewa katika hatua hii, lakini ni sehemu ya matokeo ambayo tumeyapata.

“Kikubwa mashabiki wasikatishwe tamaa waendelee kutusapoti ili tuendelee kufanya vema katika ligi na Kombe la FA na zaidi kuuchukua makombe yote,” alisema Kagere.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA GAZETI LA CHAMPIONI KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMAMOSI