Home Uncategorized KOCHA SIMBA KUIFUATA GWAMBINA FC KWA TAHADHARI

KOCHA SIMBA KUIFUATA GWAMBINA FC KWA TAHADHARI

 


 KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck ameweka wazi kwamba anaingia kwa umakini kwenye mechi yao na Gwambina FC licha ya kwamba wamekuwa na maandalizi mazuri.

 

Kocha huyo ameongeza kuwa umakini ambao anaingia nao ni kwa sababu ya kutotaka kupoteza pointi mbele ya wapinzani wake hao.

 

Mbelgiji huyo ataiongoza Simba kwenye mechi ya nne ya Ligi Kuu Bara kwa msimu huu dhidi ya Gwambina FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar itakayopigwa leo majira ya saa 1:00 usiku.

 

Sven amesema kuwa licha ya kwamba walicheza mechi moja ya kujiandaa na mechi hiyo lakini hilo haiwafanyi kutoingia kwa tahadhari mbele ya wapinzani wao hao.


“Tulicheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya African Lyon lakini haijatosha bado kutuaminisha kwamba tuko vizuri licha ya kuwa kila mchezaji kaonyesha uwezo wake mkubwa kwenye nafasi aliyocheza.

 

“Tunataka kufanya vizuri kwa mara nyingine kwenye mechi hii kwa sababu ya kufikia lengo letu la kutwaa kila pointi kwenye mechi zetu zote za hapa karibuni,” amesema.


Simba ikiwa imecheza mechi tatu za ligi imefunga mabao saba huku ikifungwa mabao mawili na wapinzani wake.


Ilianza kushinda mbele ya Ihefu FC Uwanja wa Sokoine mabao 2-1, sare ya kufungana bao 1-1 na Mtibwa Sugar na ushindi wa mabao 4-0 mbele ya Biashara United.


Inakutana na Gwambina FC ambayo bado safu yake ya ushambuliaji haijaambulia bao ndani ya dakika 270 uwanjani.


Ilianza kwa kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Biashara United, ililazimisha sare ya bila kufungana na Kagera Sugar na imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 mbele ya Gwambina FC.


Ndani ya dakika 270 imeambulia pointi moja kibindoni imefungwa mabao mawili.


SOMA NA HII  RATIBA YA TANZANIA KUFUZU MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA KWA MATAIFA YA AFRIKA