Home Uncategorized KASI YA MANCHESTER UNITED INAFURAHISHA

KASI YA MANCHESTER UNITED INAFURAHISHA


LICHA ya Junior Stanisiasi nyota wa Bournemouth kufunga bao la kuongoza dakika ya 16 halikuwazuia Manchester United kuvuna pointi tatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa Uwanja wa Old Trafford, jana.

Kasi ya United kwenye kusaka ushindi inafurahishwa kwani ni ushindi wake wa nne mfululizo. Ilianza kushinda mbele ya Sheffield United kisha Norwich ikamalizana na Brighton na jana ilikuwa zamu ya Bournemouth Julai 9 itakutana na Aston Villa ya Mbwana Samatta.

United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer ilianza kushusha mvua ya mabao kupitia kwa Mason Greenwood kinda mwenye miaka 18 aliyefunga mabao mawili dakika ya 29 na 54 huku Marcus Rashford akifunga dakika ya 35 kwa penalti, Anthony Martial dakika ya 45 na Bruno Fernandes dakika ya 59.

Bao la pili kwa Bournemouth iliyokubali kichapo cha mabao 5-2, ikiwa nafasi ya 19 na pointi 27, lilipachikwa na Joshua King dakika ya 49 kwa mkwaju wa penalti.

Ushindi huo unaifanya Manchester United kuwa nafasi ya 5 na pointi zake 55 zote zikiwa zimecheza mechi 33 ndani ya Ligi Kuu England.

Solskjaer amesema kuwa anafurahi kuona vijana wake wanafanya kazi kwa juhudi kutafuta matokeo ndani ya uwanja.

SOMA NA HII  KOBE BYRANT AZIKWA KWA SIRI