Home Uncategorized ISHU YA RAIS WA CAF KUTUA BONGO KUZINUFAISHA SIMBA NA YANGA

ISHU YA RAIS WA CAF KUTUA BONGO KUZINUFAISHA SIMBA NA YANGA


UJIO wa Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Ahmad Ahmad hapa nchini utazipa matunda mazuri klabu kongwe nchini Simba na Yanga kimataifa.

Rais huyo alikuepo uwanjani Machi 8 wakati Yanga ikiibuka na ushindi mbele ya Simba kwa bao 1-0 Uwanja wa Taifa mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Habari zinaeleza kuwa licha ya kuja kwenye ziara ya siku tatu ilikuwa ni maalumu kushuhudia ushindani wa Kariakoo dabi pale unapowakutanisha watani wa jadi namna ushindani unavyokuwa.


 “Caf ina mpango wa kuanzisha Ligi ya Afrika itakayozihusisha klabu kubwa zenye mvuto Afrika hivyo Yanga na Simba ili ziingie ni lazima zitazamwe mechi zao. 

“Ujio wa Rais wa CAF ni maalumu na uliratibiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na Yanga na Simba kwa lengo la kumshawishi Ahmad ili aweze kuziingiza timu hizo kwenye Ligi ya Afrika ambayo itazihusisha klabu zenye mvuto,”.

 Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumburi alisema :” Taarifa hizo nimezisikia lakini bado taarifa rasmi sijazipata, hivyo ni suala la kuvuta subira,”.

SOMA NA HII  DIDA; NINA OFA TANO MKONONI KWA SASA