Home Uncategorized YANGA YATUMA UJUMBE HUU KWA PAPY TSHISHIMBI

YANGA YATUMA UJUMBE HUU KWA PAPY TSHISHIMBI


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umemtumia salamu za kumtakia maisha marefu nahodha wao Papy Tshishimbi ambaye leo anatimiza miaka kadhaa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kabla ya kufanya shughuli zake leo alianza kumtumia ujumbe Tshishimbi kumtakia kheri ya kuzaliwa.

“Leo ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa nahodha wetu Tshishimbi, kabla ya kuanza kufanya harakati zozote nilimtumia ujumbe kumtakia maisha mema.

“Mashabiki pia nimeona wamekuwa wakimtakia heri nahodha wetu hili ni jambo jema pia wasisahau kuendelea kuchukua tahadhari ya kujilinda na Virusi vya Corona,” amesema.

SOMA NA HII  MBELGIJI SIMBA AMTAKA KOCHA WA MAKIPA AKASOME, LA SIVYO.......