Home Uncategorized DAVID KISSU AJIFUNGA MIAKA MIWILI AZAM FC

DAVID KISSU AJIFUNGA MIAKA MIWILI AZAM FC

DAVID Mapigano Kissu, leo Agosti 6 ametambulishwa rasmi kuwa mali ya Azam FC baada ya kusaini kandarasi  ya miaka miwili akitokea Klabu ya  Gor Mahia ya Kenya.

Kissu alikuwa sehemu ya kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kabla ya janga la Virusi vya Corona halijasimamisha masuala mengi duniani ikiwa ni pamoja na masuala ya michezo.

Kipa huyo alichezea timu za Njombe Mji na Singida United, kabla ya kutimkia nchini Kenya. Akiwa na Gor Mahia, amecheza jumla ya mechi 15, huku akiwa hajaruhusu nyavu zake kuguswa (clean sheet) katika mechi tisa kati ya hizo na timu yake ilitangazwa kuwa mabingwa wa ligi ya Kenya.

Kissu anakamilisha idadi ya nyota watano ambao wamesajiliwa ndani ya Azam FC na tayari imeshaanza mazoezi ya maandalizi ya msimu wa 2020/21 wengine ni Awesu Awesu, Ally Niyonzima, Ayoub Lyanga na Ismail Aziz Kada.
SOMA NA HII  SIMBA: MCHEZO WETU UTAKUWA MGUMU, MASHABIKI WATUPE SAPOTI