Home Uncategorized SIMBA QUEENS YACHEKELEA UBINGWA WA LIGI YA WANAWAKE

SIMBA QUEENS YACHEKELEA UBINGWA WA LIGI YA WANAWAKE


Pichani:-Nahodha na Mshambuliaji wa Simba Queens, Mwanahamis Omary (kulia), akimtoka beki wa Baobab Queens, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliochezwa leo Agosti 5 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Simba Queens ilishinda mabao 5-0. (Picha na George Mganga).


MWANAHAMIS Omary, nahodha na mshambuliaji wa Klabu ya Simba Queens, amesema kuwa ni furaha kwa timu na uongozi kiujumla kwa timu yao kutwaa taji la kwanza kwa msimu wa 2020/21 kwenye Ligi ya Wanawake.

Ushindi wa mabao 5-0 mbele ya Baobab Queens kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake uliochezwa Uwanja wa Uhuru umeipa tiketi timu ya Simba Queens kuwa mabingwa wakiwa na mechi mbili mkononi.

Inafikisha jumla ya pointi 53 ambazo haziwezi kufikiwa na  JKT Queens ambao ni mabingwa watetezi ipo nafasi ya pili na pointi 46 huku Baobab Queens ikiwa nafasi ya nane na pointi 22 zote zimecheza mechi 20.

Mwanahahamisi amesema:”Msimu uliopita tulipambana ila tulishindwa kutwaa ubingwa, kwenye usiku wa tuzo za Mo niliwaambia viongozi kuwa ikiwa watawekeza na nguvu huku kwetu pia basi tutafikia mafanikio ambayo wanahitaji ndicho kilichotokea.

“Nina furaha kutwaa ubingwa nikiwa na Simba na ninaipenda timu yangu na kazi pia, shukrani kwa mashabiki na viongozi kwa sapoti ambayo wanatupa waendelee kufanya hivyo na kwenye mechi zetu mbili tukakwenda kufanya kazi ya ushindani hatujaridhika bado licha ya kuwa ni mabingwa.”
SOMA NA HII  MUUAJI WA SIMBA AMTAJA MKE WAKE KUHUSIKA KWENYE MABAO YAKE YOTE NDANI YA YANGA