Home Ligi Kuu WANAUME LEO KAZINI KWENYE MECHI ZA MAAMUZI

WANAUME LEO KAZINI KWENYE MECHI ZA MAAMUZI


 WANAUME watakuwa kazini leo kwenye mechi za machozi na tabasamu ambalo litatokana na matokeo baada ya dakika 90.


Ukweli ni kwamba mechi zote za leo ikiwa ni lala salama zitakuwa ni ngumu kwa kila timu kwa kuwa zimeshikilia maamuzi ya msimu mzima hasa kwa hesabu za timu ambapo zilianza na sasa zinakwenda kumaliza hesabu zao.


Kwa kete ya leo ambayo itachezwa itatoa picha kamili ya msimu ujao kwa timu ambazo zitabaki ndani ya ligi pamoja na zile ambazo zitamaliza ndani ya nne bora ambapo ni timu moja pekee ina uhakika wa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza kwa sasa ambayo ni Mwadui FC iliyo nafasi ya 18 na pointi zake 19.


Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Tanzania, Karim Boimanda amesema kuwa mechi zote zinafuatiliwa ili kuepuka ule ujanjaunjaja katika lala salama.


Pia kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya waamuzi Tanzania, Sud Abdi Mohamed amesema kuwa waamuzi wameambiwa wachezeshe mpira kwa kufuata sheria 17.


Cheki mechi za leo zitakavyokuwa za maamuzi kwa timu zitakazoshuka uwanjani:-


Tanzania Prisons v Biashara United


Tanzania Prisons inayonolewa na Kocha Mkuu, Salum Mayanga ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya  Biashara United, Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.


Ikiwa ipo nafasi ya 8 na pointi zake 42 hesabu zake ni kumaliza ndani ya 10 bora ikijichanganya inaweza kushushwa na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 9 na pointi 42 wakitofautiana kwa idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa. Muziki wake ni dhidi ya Biashara United ambayo inasaka pointi moja ili kufikisha pointi 50 zitakazoamua imalize ikiwa nafasi ya nne.


KMC v JKT Tanzania


KMC iliyo nafasi ya 6  inahitaji kumaliza ndani ya tano bora matokeo ya leo yatatoa maamuzi juu ya ndoto hizo ambapo inakutana na  JKT Tanzania iliyo nafasi ya  14 na pointi 36 ikiwa inapambana kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja itakuwa ni Uwanja wa Uhuru, Dar.


Ruvu Shooting v Namungo


Ruvu Shooting iliyo nafasi ya 10 na pointi 38 haina uhakika wa kubaki ndani ya ligi ikiwa itatayeyusha pointi tatu leo mbele ya Namungo iliyo nafasi ya tano na pointi 43, itapigwa Uwanja wa Mabatini, Pwani.

SOMA NA HII  MTAMBO WA MABAO NDANI YA NAMUNGO FC NJE YA UWANJA MIEZI MITATU


Ili ihakikishe inatimiza lengo la kubaki ndani ya ligi lazima ishinde kwa kuwa alama alizonazo zinaweza kufikiwa na Coastal Union  iliyo nafasi ya 17 na pointi zake 34 huku Namungo wao wakihitaji kumaliza ndani ya 5 bora.


Mbeya City v Gwambina


Mbeya City ipo nafasi ya 13 ina pointi 36 inakutana na Gwambina FC iliyo nafasi ya 16 na pointi 34, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.


Zote hazina uhakika wa kubaki ndani ya ligi msimu ujao hivyo mechi za leo zitatoa maamuzi nani atatanguliza mguu moja Ligi Daraja la Kwanza na nani atakuwa kwenye nafasi ya kucheza mechi za mtoano.


Polisi Tanzania v Kagera Sugar


Polisi Tanzania ipo nafasi ya 7 hesabu zake ni kuona inamaliza ndani ya tano bora kibindoni ina pointi 42 inakutana na  Kagera Sugar yenye pointi 37 ipo nafasi ya 12 ikipambana kujinasua kutoka kwenye hatari ya kushuka daraja. Ngoma hii itapigwa Uwanja wa Ushirika, Moshi.


Coastal v Mwadui


Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 9 na pointi zake 42 inahitaji kumaliza ndani ya 10 bora  inakutana na Mtibwa Sugar inayopambania kubaki ndani ya ligi ikiwa ipo nafasi ya 11 na pointi 38, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.


Coastal Union inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda ipo nafasi ya 17 ina pointi 34 inakutana na  Mwadui FC iliyo nafasi ya 18 na pointi 19 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


Zote zipo kwenye mstari mwekundu ambapo Mwadui FC hesabu zinaigomea kubaki ndani ya ligi, Coastal Union wao wanapambana kuona nini watavuna mbele ya Mwadui FC inayotafuta maamuzi ya heshima leo.


Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 70 inakutana na kigongo cha Ihefu FC ambayo inapambana kujinasua kushuka daraja ikiwa nafasi ya 15 na pointi 35, Uwanja wa Mkapa Dar.


Azam v Simba


Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi zake 64 inahitaji kumaliza kwa heshima ndani ya tatu bora  inakutana na Simba ambao ni mabingwa wa ligi kwa msimu wa 2020/21, Uwanja wa Azam Complex, Dar.


Itahitaji kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wao wa Kombe la Shirikisho, Songea kwa kuwa walifungwa bao la harakaharaka Uwanja wa Majimaji sasa watakuwa nyumbani.