Home Uncategorized KOCHA MWADUI FC ALIYEPIGWA 5G NA YANGA AFUTWA KAZI

KOCHA MWADUI FC ALIYEPIGWA 5G NA YANGA AFUTWA KAZI


 IMEELEZWA kuwa uongozi wa Mwadui FC umemfuta kazi Kocha Mkuu wa timu hiyo Khalid Adam kutokana na mwendo mbovu wa timu yake.


Adam amekiongoza kikosi cha Mwadui FC kwa msimu wa 2020/21 ndani ya Ligi Kuu Bara kwenye jumla ya mechi 15 na imeshinda mchezo mmoja pekee ndani ya ligi.


Mechi 11 amepoteza na kuambulia sare moja huku timu hiyo ikiwa nafasi ya 18 baada ya kukusanya pointi 10.


Mchezo wake wa mwisho kukaa benchi ilikuwa Desemba 12 ambapo alipokea kichapo cha mabao 5-0 dhidi ya Yanga ikiwa ni ushindi mkubwa kwa Yanga inayonolewa na Cedric Kaze kwa msimu huu.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Mwadui FC David Chakala amesema kuwa bado hajapata taarifa rasmi kuhusu kufutwa kazi kwa Adam hivyo hawezi kutoa taarifa rasmi.


“Leo hatukuwa na mazoezi kwa sababu hatukuwa na mechi ila kesho ndo itakuwa siku ya kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mechi zetu zijazo za ligi.


“Mwalimu nimemuona hapa ila hakuwa na timu kwa kuwa hakukuwa na mazoezi labda mpaka kesho nikipata taarifa nitajua ni nini ninaweza kuzungumzia ikiwa kutakuwa na taarifa nyingine,” .

SOMA NA HII  HUYU HAPA ATAJWA KUWA NYUMA YA UBORA WA MARTIAL WA MANCHESTER UNITED