Home Uncategorized HUYU HAPA ATAJWA KUWA NYUMA YA UBORA WA MARTIAL WA MANCHESTER UNITED

HUYU HAPA ATAJWA KUWA NYUMA YA UBORA WA MARTIAL WA MANCHESTER UNITED


IMEELZWA kuwa ubora wa Anthony Martial ndani ya Manchester United unazidi kuimarika tofauti na awali kutokana na ujio wa nyota mpya ndani ya kikosi hicho.

Gwiji wa Klabu ya Manchester United, Roy Keane amesema kuwa ubora wake unatokana na ujio wa mshambuliaji mpya, Odion Ighalo.

Ighalo alijiunga na United ili awe mbadala wa Rashford ambaye ni majeruhi akitokea Klabu ya Shanghai Shenhua ya China kwa mkopo na ametupia mabao matatu.

Keane amesema ujio wa Ighalo umeongeza umakini na utulivu kwa Matial ambaye amepata mpinzani wake.


 “Muda mwingine mshambuliaji anapokuja mnampa pongezi na anawainua wengine akipambana, Martial amejibu baada ya kufikiri kwamba amepata mchezaji mwingine wa kupambania namba hili ni jema,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA YATAJA SIRI YA MAFANIKIO, HESABU ZAO NI MBELE YA NAMUNGO