Home news A-Z KUHUSU SAKATA LA AJIBU KUONDOKA KAMBINI NA KUACHANA NA SIMBA MAZIMA

A-Z KUHUSU SAKATA LA AJIBU KUONDOKA KAMBINI NA KUACHANA NA SIMBA MAZIMA


WIKI moja kabla ya fainali ya Kombe la Shirikisho (ASFC) dhidi ya Yanga itakayopigwa Julai 25, kambi ya Simba imeanza kumeguka baada ya mshambuliaji wao, Ibrahim Ajibu kuamua kujichomoa jumla kambini baada ya kushtukiwa na viongozi wake kuwa amemalizana na watani wao wa Jangwani.

Inaelezwa kuwa, nahodha huyo wa zamani wa Yanga ameondoka mazima hajaacha hata soksi, hasa baada ya kugundua viongozi wake wamemkaushia na kutomtaka kabisa kikosini, naye akaamua kujiongeza. Hata hivyo, taarifa za kutimka kambini kwa Ajibu zimefanywa siri, ikielezwa ana matatizo la kiafya, lakini japo watu wake wa karibu wakieleza mshambuliaji ndio basi kwani tayari ameshaaga kabisa akijiandaa kuanza maisha mapya katika timu nyingine kwa msimu ujao.

Iko hivi. Wachezaji wa Simba hata wakipewa mapumziko ya muda mrefu huwa wanaacha vifaa vyao vya mazoezi katika vyumba vya kambini kwao eneo ya Bunju, lakini siku kadhaa zilizopita Ajibu alikwenda katika kambi hiyo na alichukua kila kilicho chake kisha akaondoka navyo.

Taarifa inaelezwa Ajibu alizinguana na mabosi wake naye kuamua kuchukua kila kinachomhusu, huku akipeleka karatasi inayoonyesha amefanya vipimo kwa meneja wa timu, akidai anaumwa malaria, lakini karatasi hiyo ya hospitali ilikuwa ya x-ray kitu kilichowashangaza na kuwachefua. Benchi la Ufundi la Simba, halikufurahishwa na jambo hilo, kwa kubaini wamepigwa fiksi kupita kiasi na kumfanya Kocha, Didier Gomes kumtaka Meneja Patrick Rweyemamu kuwasiliana tena na mchezaji ili arudi kambini.

Meneja aliwasiliana na Ajibu siku ya kwanza tu, alipomwambia hata kama anaumwa anatakiwa kuwepo kambini lakini tangu hapo hadi unasoma hapa hawapokelei simu viongozi wake.

Inaelezwa Rweyemamu mbali ya kumpigia simu bila ya kupata majibu yoyote kwa Ajibu ambaye hapokei simu huwa anawauliza marafiki zake, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ na wengineo alipo mwenzao lakini hakuna jibu kamili.

Rweyemamu baada ya kufanya juhudi zote hizo bila ya majibu, alimrudishia majibu, Gomes jitihada zake za kumtafuta Ajibu zimegonga mwamba kwani hakuna alicho fanikiwa.

SOMA NA HII  WAKATI HUKU YANGA WALIMUONA KITUKO..SARPONG AWA LULU UARABUNI..KULIPWA TSH MIL 27 KWA MWEZI

Baada ya hapo, Gomes pamoja na Rweyemamu walifikisha jambo hilo kwa Ofisa mtendaji mkuu, Barbara Gonzalez ambaye naye alianza kufanya juhudi za kumtafuta.

Barbara kwa nyakati tofauti amekuwa akimpigia simu na kumtumia ujumbe mfupi, Ajibu ambaye amekuwa hapokei na kuacha kujibu ujumbe huo mfupi hadi wakati huu.

Jambo hilo limewakera viongozi wa Simba pamoja na benchi la ufundi rasmi wameamua kumtoa katika mipango yao ya msimu huu na hawatakuwa tayari kumuongezea mkataba mpya licha ya kuwa mchezaji kipenzi ya mmoja wa vigogo mwenye nguvu.

AJIBU MWENYEWE

Gazeti la Mwanaspoti baada ya kupata picha nzima kwa upande wa Simba, limebaini kuwa, Ajibu amesaini mkataba wa awali na Yanga, japo kuna taarifa huenda akaibukia KMC wanaoonekana kuhitaji zaidi huduma yake. Chanzo kilichopo karibu na Ajibu, anayefanya kazi ofisi za GSM, kimeeleza amemshuhudia nyota huyo akimalizana na Yanga, japo baadhi ya vigogo waligawanyika juu ya usajili wake huo.

YANGA SASA

Taarifa za chinichini ndani ya Yanga kuna mgawanyiko mkubwa, kweli Ajibu amechukua mpunga wa kusaini mkataba, lakini viongozi wamegawanyika katika jambo lake.

Kuna wimbi kubwa la viongozi ambao hawataki kumuona Ajibu anarudi tena kucheza katika kikosi hicho, lakini kuna wengine wanajaribu kumtetea ili acheze msimu ujao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here