Home Yanga SC WACHEZAJI SABA WA YANGA LEO KUIKOSA IHEFU KWA MKAPA

WACHEZAJI SABA WA YANGA LEO KUIKOSA IHEFU KWA MKAPA


 YANGA inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasredddine Nabi leo Julai 15 inakibarua cha kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Ihefu FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Zuber Katwila.

Nabi anatarajia kuwakosa nyota wake 7 kutokana na sababu mbalimbali. Nyota hao ni pamoja na Yassin Mustapha ambaye bado hajarejea kwenye ubora wake kwa kuwa alikuwa anatibu majeraha.

Abdalah Shaibu, ‘Ninja’ huyu pia bado hajarejea kwenye ubora kwa kuwa alikuwa anatibu majeraha.

Metacha Mnata, kipa namba moja wa Yanga ishu yake ya nidhamu baada ya kuonyesha ishara ya matusi kwa mashabiki kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting.

Fiston Abdulazack kiungo huyu mshambuliaji dili lake la miezi sita limemeguka na aliweka wazi kwamba anarejea Burundi.

Michael Sarpong pamoja na Lamine Moro hawa ishu ya nidhamu iliwaweka kando ya kikosi hicho pamoja na Mapinduzi Balama ambaye huyu ni mgonjwa wa muda mrefu. 

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Ihefu inakumbuka mchezo wao uliopita walipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 pia nafasi ambayo wapo ni kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja.

Ihefu ipo nafasi ya 15 na pointi zake ni 35 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi zake ni 70.


SOMA NA HII  YANGA WAINGIA HOFU DHIDI YA NAMUNGO...KIKAO KIZITO CHAFANYIKA..WACHEZAJI WATOKA WAKICHEKA....