Home Habari za michezo WAKATI NABI AKIWASILIZIA KAIZER CHIEF….MORRISON AIBUKA NA KUINGILIA DILI KWA NYUMA…

WAKATI NABI AKIWASILIZIA KAIZER CHIEF….MORRISON AIBUKA NA KUINGILIA DILI KWA NYUMA…

Habari za Yanga SC

Huku Nasreddine Nabi akitarajiwa kutangazwa muda wowote kuwa kocha wa Kaizer Chiefs, nyota wa zamani wa Ligi ya Afrika Kusini (PSL), Bernard Morrison amefanya ulinganisho kati ya Amakhosi na Yanga, ambayo anaichezea kwa sasa.

Licha ya kupitia kipindi kigumu, Kaizer Chiefs imesalia kuwa miongoni mwa timu zinazofuatiliwa kwenye ligi ya Afrika Kusini.

Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye vituko vingi nje ya uwanja, alisema Yanga, ambayo ni bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Kombe la ASFC na wanafainali wa Kombe la Shirikisho Afrika ni wakubwa kuliko Kaizer Chiefs.

Morrison alikaa Afrika Kusini kwa miaka miwili akiichezea Orlando Pirates kabla ya kuondoka Julai 2018.

Alikaa mwaka mmoja Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na baadaye akatua Yanga, Januari 2020, kabla ya kwenda Simba na kurejea tena.

“Namba za klabu (Yanga) ni zaidi ya Kaizer Chiefs. Kwenda Kaizer Chiefs kunakuja na shinikizo lake,” alisema Morrison, ambaye alifanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari cha Afrika Kusini.

“Lakini kama mchezaji, lazima utoe. Kuchezea klabu kubwa maana yake ni lazima uwe tayari kwa kila jambo.

“Kama unahama kutoka Yanga na kwenda Afrika Kusini kuchezea Kaizer Chiefs, lazima uwe tayari. Kwangu mimi nadhani presha kubwa ipo Tanzania zaidi kuliko hata ile ya Afrika Kusini.

“Hata Kaizer Chiefs wanapokwenda kucheza ugenini, hawapati umati huu mkubwa. Lakini hapa unapata namba kubwa kila wakati unapokwenda kwenye mechi. Lazima uwe tayari.”

Chini ya kocha ya Nabi, Yanga imeshinda mataji sita katika misimu miwili, Ligi Kuu mara mbili, mawili ya Kombe la FA (ASFC) na Ngao ya Jamii mara mbili.

SOMA NA HII  HAWA HAPA MASTAA WA TIMU YA TAIFA WALIPATA SHAVU LA KUSAJILI UTURUKI...