Home Habari za michezo SIMBA KWENDA ZNZ KUCHUKUA ‘DAWA’ YA KUWAMALIZA AL AHLY ….MASTAA HAWA KUKOSEKANIKA…

SIMBA KWENDA ZNZ KUCHUKUA ‘DAWA’ YA KUWAMALIZA AL AHLY ….MASTAA HAWA KUKOSEKANIKA…

Habari za Simba leo

KIKOSI cha Wekundu wa Msimbazi, Simba kinaondoka leo kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki mbili na kucheza mechi moja ya kirafiki kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly.

Katika mchezo huo Simba wataanzia nyumbani Machi 29, mwaka huu, wakiwakaribisha Al Ahly ya Misri uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam, saa 3:00 Usiku.

Kwa mijibu wa Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema sababu kubwa mbili ambazo Kocha Abdelhak Benchikha kutaka kambi hiyo ikiwemo kupaga utulivu wa kuandaa program ya kikosi chake na kupata muda wa usiku kufanya maandalizi hayo.

Amesema wachezaji wote watasafiri kasoro wale walikuwepo katika majukumu ya timu za Taifa akiwemo Clatous Chama, Saidi Ntibazonkiza, Henock Inonga na wazawa ni Aishi Manula, MohammedHussein, Kennedy Juma na Kibu Denis.

“Baada ya mechi na Mashuja FC, wachezaji walipata mapumziko mafupi na wanarejea kesho(leo) kuanza maandalizi makubwa kwa ajili ya mambo mawili katika mchezo wetu dhidi ya Al Ahly.

Jambo la kwanza kuwatoa Al Ahly katika hatua hii suala la kuwafunga hilo tumefanya sana kwa sababu ndani ya miaka mitano tunekutana nao mara tatu katika michezo sita tumeshinda mara mbili. Kufungwa mara mbili na sare pia, hivyo hivyo kwa Al Ahly, “ amesema Ahmed.

Ameeleza kuwa wanataka kutengeneza mipango mizuri na maandalizi ‘bab kubwa’, kwa ajili ya kumuondoa Al Ahly katika hatua ya robo fainali msimu huu wamedhamilia kuingia nusu fainali.

SOMA NA HII  KUMBE! ONYANGO HAJUI KUHUSU KUHITAJIKA NA TIMU YA AFRIKA KUSINI