Home Habari za michezo SIMBA WAAANZA KUCHOMOA MMOJA MMOJA YANGA….KIBABAGE ATAJWA KWENYE DILI…

SIMBA WAAANZA KUCHOMOA MMOJA MMOJA YANGA….KIBABAGE ATAJWA KWENYE DILI…

Habari za Michezo leo

Klabu ya soka ya Singida Fountain Gate imethibitisha kupokea ofa ya Klabu ya Simba juu ya kuhitaji huduma ya mlinzi wake kushoto, Nickson Kibabage.

Hii ni baada ya taarifa kusambaa kuwa Simba SC imeanza mazungumzo ya kumsajili Kibabage anayekipiga kwa mkopo kwenye Klabu ya Yanga SC.

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari Singida Fountain Gate, Hussein Masanza amesema; “Issue ya Kibabage ni kweli Simba wameutafuta uongozi kuonesha nia ya kutaka saini yake.

“Bado ni mapema sana kuzungumzia lakini nathibitisha ni kweli jambo hilo lipo na sio dhambi kuwepo. Hakuna muafaka uliofikiwa bado. Kama kutakuwa na lolote klabu itatoa taarifa,” amesema Masanza.

Lunyasi wanamuona Kibabage kama mbadala wa muda mrefu wa mlinzi wa kushoto wa klabu hiyo Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Simba wanamhitaji Kibabage kwenda kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa mashindano na kumpatia kocha Benchikha kikosi kipana kwa ajili ya kurudisha mataji ambayo Simba wameyakosa kwa misimu miwili mfululizo.

Mkataba wa Singida na kibabage utaisha 2025, na atarejea katika kikosi cha Singida baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo kwa wananchi mwishoni mwa msimu huu.

SOMA NA HII  WAKATI MAMBO YAKIWA MAGUMU KWAKE TOKA ASAJILIWE...AMBANGILE AFUNGUKA HAYA KUHUSU CHICO USHINDI...