Home news MANARA AFUNGUKA SAKATA LA SHAFFIH DAUDA KUFUNGIWA…ADAI NI USHENZI NA USHAMBA..AITAJA SIMBA..

MANARA AFUNGUKA SAKATA LA SHAFFIH DAUDA KUFUNGIWA…ADAI NI USHENZI NA USHAMBA..AITAJA SIMBA..

Licha ya Kushambuliana katika mitandao ya Kijamii mara kwa mara kati ya Msemaji wa Klabu ya Yanga na Mchambuzi wa Soka kutoka kituo cha Redio cha Clouds Fm Shaffih Dauda, hilo halimfanyi kuwa na fikra mbaya juu ya Mchambuzi huyo.

Siku ya Jana Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF, ilitoa taarifa ya Kumfungia Shaffih Dauda kujiuhisha na Soka kwa miaka mitano ndani na nje na kulipa faini ya Shilingi milioni 6.

Sasa Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram amezungumzia suala hilo, ambapo Haji ameandika;

“Jana nilipoona hii taarifa usiku ilinistua sana na kunifadhaisha mno ,,huwa najisikia shida nikiona mtu nimjuae akiingia katika matatizo yoyote yale no matter wat,,,

Binadamu hatupaswi kufurahia pale mwenzetu anapopata mitihani au vtu kama hv,,ingawa baadhi yetu tumekuwa na desturi ya kufurahia shida za Watu na wakati mwingine kuombeana mabaya kabisa

Inafika muda mtu anaweka kabisa post ya kutaka mtu anaemjua kabisa afungiwe au hata afungwe jela au kushtakiwa,,,hii sio uungwana ndugu zangu,,na tujue shida na matatizo hayana mmoja na sote hatuijui kesho yetu,,,

Nakumbuka vzuri nilipoondoka Simba ,,baadhi ya watu ninaowafahamu na ambao hata kuchill sometimes tunachil wote,jinsi walivyofurahia na kuandika makala moto moto za hadi kusema nimekwisha ,,Wengine walienda mbali zaidi na kusema sitaajiriwa kokote,,na ntapoteza endowments zangu zote za kibiashara,,utadhani wao ndio wagawa rizki au Manaibu Mungu vile!!

Hv,unawezaje kibinadaamu Mhangaikaji mwenzio na mpo wote ktk tasnia ya football,,ukapost video ya mtu wa mtaani anasema Fulani anapaswa kushtakiwa au afungwe jela na hafai kuwemo ktk Soka,,,,Mpira huu huu au vita ndugu zangu? Tupende kuweka akiba Mabibi na Mabwana!! Sote tunahitajiana kwa hili au lingine ,,

Mtu umepata kifursa kidogo cha kusikika redioni basi kutwa kutaka wenzio waharibikiwe,,unatumia kipindi cha masaa zaidi ya mawili kumsema binadamu mwenzako,,tena unazishangaa mamlaka za Soka kwa kumpiga faini binadamu mwenzio,badala ya kumfungia,,,au kutaka Polisi wakamate wenzio kisa nn ? Punguzeni hzo roho watu wangu,,tuna kesho yetu tusiyoijua

SOMA NA HII  YANGA:-"FEI TOTO ACHA UJEURI...HUWEZI KUSHINDANA NA KLABU...ISHU NZIMA IKO HIVI A-Z

Tusipende kuombeana mabaya kwa kuwa tu tunatofautiana mitazamo ya kikazi au ya kishabiki wa mpira,, Mm kwangu naona huo ni ushenzi na ushamba,,na ktk jambo hili la ndugu yangu huyu,,kutoka moyoni namuombea kwa Mungu na naamini litaisha,,cc watu wa mpira ni wasamehevu na naamini TFF (@tanfootball) wanazungumzika kwa maslahi makubwa ya football.

Pole bro na naamini jambo lako litaisha kwa amani’