Home Uncategorized YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA JKT TANZANIA

YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA JKT TANZANIA


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ushindani na wana amini kuwa watapata pointi tatu leo mbele ya JKT Tanzania.

Yanga itamenyana na JKT Tanzania majira ya saa 10:00 jioni Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

“Wachezaji wapo sawa na morali yao ipo kamili kwa ajili ya ushindani, nina amini tutapata matokeo chanya kwani tunahitaji pointi tatu,” amesema.

Mchezo uliopita uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Yanga iliwatungua mabao 3-2 JKT Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed,’Bares’.

SOMA NA HII  KAGERA SUGAR INA MAJEMBE 8 YA KAZI, MOJA KUTOKA YANGA, HAWA HAPA