Home Uncategorized SIMBA: WAJEDA WALITUZIDI KWENYE UIMARA, TUNASAHAU MATOKEO TUNAENDELEA KUPAMBANA

SIMBA: WAJEDA WALITUZIDI KWENYE UIMARA, TUNASAHAU MATOKEO TUNAENDELEA KUPAMBANA

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa haikuwa rahisi kupambana na Ruvu Shooting kwa kuwa ni timu ya jeshi iliwazidi kwenye upande uimara.

Ruvu Shooting, ililazimisha sare mbele ya Simba, Juni 14 Uwanja wa Taifa kwa kufanya ubao usomeke 1-1 baada ya Shiza Kichuya kuanza kufunga bao huku wao wakiweka usawa kupitia kwa Fully Maganga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Sven amesema kuwa wachezaji wake walikuwa na muda mfupi wa mazoezi jambo ambalo liliwafanya wasiwe na utimamu kimwili.

“Wapinzani wetu walikuwa wanajeshi sasa unapozungumzia wanajeshi ipo wazi kwamba wanatakiwa kuwa bora muda wote hapo ndipo ambapo walituzidia kwani wachezaji wangu hawakuwa na muda mrefu wa kufanya mazoezi.

“Nina amini kwamba walipambana ndani ya uwanja ila matokeo ndio yalikuwa namna hiyo, hakuna kilichoharibika tunatazama mechi zinazofuata,” amesema.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 72 baada ya kucheza mechi 29 za ligi,Juni 20 itamenyana na Mwadui FC Uwanja wa Taifa.

SOMA NA HII  SINGIDA YA KIMATAIFA NJE YA DIMBA