Home Uncategorized DILI LA RUTANGA YANGA HAWA WAMEHUSIKA KUMPA MIAKA MIWILI

DILI LA RUTANGA YANGA HAWA WAMEHUSIKA KUMPA MIAKA MIWILI

ERIC Rutanga alisaini kandarasi ya awali na Klabu ya Polisi Rwanda licha ya kuhusishwa kuibukia ndani ya Yanga.

Rutanga amesema kuwa kule alisaini mkataba wa awali ambao unampa ruhusa ya kufanya mazungumzo na timu nyingine. 
Beki huyu wa kushoto anayekipiga ndani ya Klabu ya Rayon Sports inaelezwa kuwa ameshamalizana na Yanga kwa dili la miaka miwili.

Meneja wa mchezaji huyo, Herve Tra Bi amesema kuwa wameshamalizana na mabosi wa Yanga. “Tayari tumeshamalizana na mabosi wa Yanga, Hersi Said, Arafat Haji kutoka GSM ndio tuliokuwa katika mipango ya kuhakikisha tunakamilisha usajili wa Eric Rutanga lakini bila kumsahau Kocha, Luc Eymael,” .

SOMA NA HII  KOCHA YANGA ATAJA SABABU ZITAKAZOWAPA UBINGWA