Home Uncategorized WACHEZAJI WA ARSENAL WANANYOSHWA KWA KUFANYA USAFI NA ARTETA

WACHEZAJI WA ARSENAL WANANYOSHWA KWA KUFANYA USAFI NA ARTETA


MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal inaripotiwa kuwa amekuwa akiwapa adhabu ya kufanya usafi chumba cha kubadilishia nguo wachezaji wake wote ambao watavunja taratibu alizoziweka.

Adhabu za Arteta huwa hazichagui mchezaji anayepaswa kupewa wakati mwingine nahodha wa Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang amekuwa akikutana na adhabu hizo.

Lengo la kufanya hivyo ni kulinda nidhamu za wachezaji wake wote na inafanya wengi wafuate taratibu hizo na wakati mwingine huadhibiwa kwa kutakiwa kuosha gari la nahodha wa timu hiyo Aubameyang.


Makosa makubwa ambayo anayatazama Arteta inatajwa kuwa ni pamoja na mchezaji kuchelewa kwenye kikao pamoja na mazoezi.

SOMA NA HII  NAMUNGO KUSAJILI WACHEZAJI 20