Home Uncategorized YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA RUVU SHOOTING KWA MKAPA

YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA RUVU SHOOTING KWA MKAPA


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Mkapa kwa kuwa mwalimu Cedric Kaze amekiandaa kikosi kwa umakini.

Ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 31 inakutana na Ruvu Shooting yenye pointi 23 ikiwa nafasi ya nne na zote zimecheza jumla ya mechi 13 ndani ya Ligi Kuu Bara.

Tangu msimu wa 2010/11 zimekutana mara 18,Yanga imeshinda mara 13 na Ruvu Shooting ilishinda mara moja huku zikipatikana sare nne ndani ya uwanja kwenye mechi za ligi.

 Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu kipo sawa ni jambo la kusubiri wakati ili kuona namna itakavyokuwa.


“Mwalimu amekiandaa kikosi chake na kipo sawasawa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting, tunaamini kwamba utakuwa na ushindani mkubwa na wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wetu.


“Kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao kwani lengo letu ni kuona kwamba tunafikia malengo ambayo tumejiwekea ya kutwaa ubingwa,” amesema. 


Mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku.

SOMA NA HII  AZAM FC YAANZA KUWALIA MINGO WAZIMBABWE, KUKIWASHA LEO UWANJA WA CHAMAZI