Home Habari za michezo MSUVA AFUNGUKA ISHU YA KUTAKIWA SIMBA NA YANGA…AGUSIA DILI LAKE NA WAARABU...

MSUVA AFUNGUKA ISHU YA KUTAKIWA SIMBA NA YANGA…AGUSIA DILI LAKE NA WAARABU LILIVYO…


Mshambuliaji wa Taifa Stars, Simon Msuva amezima uvumi wa kuzitumikia klabu kongwe za Simba na Yanga akisema hana mpango wa kucheza soka nchini kwasasa.

Msuva amesema ingawa anahitajika na klabu nyingi za ndani na nje ya nchi lakini hana hesabu za kurejea kucheza nchini kwasasa.

“Hapa Tanzania hapana sina hesabu hizo kwasasa nina ofa nyingi lakini hapa nchini siwezi na sina hiyo akili kabisa,” amesema Msuva.

Akielezea mgogoro wake na klabu yake ya Wydad Athletic ya Morocco Msuva amesema anaamini wakati wowote kutoka sasa atapata timu ya kutunza kiwango chake wakati akisubiri uamuzi wa kesi yake.

Mshambuliaji huyo ambaye jana ameichezea Stars amewatoa hofu mashabiki wa soka akisema atamaliza kiu ya wengi wanaotaka kujua ni timu gani ataitumikia.

“Najua watu wengi wana kiu ya kujua ni wapi nitakwenda,nafikiri kiu hiyo nitaimaliza muda si mrefu nadhani baada ya muda mfupi nitajua wapi nakwenda kucheza kwa ajili ya kujiweka sawa.”

Msuva jana amerejea uwanjani akiichezea Stars kwa dakika 45 katika mchezo wa kirafiki wa kelenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya kati,ambapo katika ushindi wa mabao 3-0 amefanikiwa kutoa pasi ya bao la mwisho katika mchezo huo.

SOMA NA HII  BAADA YA SIMBA KUANZA MCHAKATO WA UWANJA WAO..YANGA NAO WAJIBU MAPIGO... SENZO 'AWAKA'...